Wednesday, March 13, 2013

Mfahamu Papa Francisco wa I

George Mario Bergoglio-Papa Fransisco wa Kwanza
Jorge Mario Bergoglio,aliyezaliwa December 17, 1936 ndiye Papa mpya wa Kanisa Katoliki Duniani na Khalifa wa Mtakatifu Petro, amechaguliwa leo Tarehe 13.03.2013  na kuchukua jina la kichungaji la Papa Francico wa Kwanza, kabla ya kuchaguliwa kuwa Papa alikuwa Kardinali wa kanisa Katoliki nchini Argentina, alihudumu kama Askofu Mkuu wa Jimbo la Buenos Aires tangu mwaka 1998 na alipata cheo cha Kardinali mnamo mwaka 2001

Maisha yake

Jorge Bergoglio alizaliwa Buenos Aires, ni mmoja kati ya watoto watano watano wa  Baba wa kiItaliano aliyekuwa akifanya kazi katika Shirika la Reli nchini humo na mkewe. Baada ya kumaliza masomo yake ya Seminari huko Villa Devoto alijiunga na jumuiya ya Yesu Kristo mwezi Machi mwaka 11.03.1958 Bergoglio alijipatia shahada ya juu ya Filosofia katika chuo cha  Máximo San José huko San Miguel, na baadaye alifundisha Fasihi na saikolojia katika chuo cha Colegio de la Inmaculada huko Santa Fe, na chuo cha Colegio del Salvador huko Buenos Aires. alipata daraja takatifu la upadre  Desemba 13, 1969, aliopewa na Askofu Ramón José Castellano. alisomea masomo ya filosofia na Teolojia huko San Miguel.Bergoglio aliendelea huvyo na kuwa Professor wa Teolojia 

Papa Fransisco wa I akiwasalimia waamini wa Kanisa Katoliki na kutoa Baraka zake za kwanza kama Baba Mtakatifu huko Vatican
Kutokana na uongozi wake mzuri Jumuiya ya Kristo ilimteua Bergoglio kiongozi toka mwaka 1973 hadi 1979, mwaka 1980 alihamishwa na kuwa Rector katika Seminary ya San Miguel ambako alisomea pia . alihudumu katika Seminari hiyo hadi mwaka 1986

Bergoglio alipata daraja la Askofu mkuu tarehe 28.02.1998 huko Argentina, Papa John Paul wa II alimwita Vatican Askofu huyo mpya tarehe 21.02.2001 na kumpa heshima kuwa Kardinali wa Argentina.


 Kabla ya Kuteuliwa kuwa Baba Mtakatifu, Kardinali George Mario Bergoglio alishika nafasi mbalimbali za uongozi wa kanisa huko Roma na katika nchi yake pia, hivyo uongozi wake ulikubalika kwanzia nchini kwake na hata katika uongozi wa kaniza zima huko Vatican.











No comments:

Post a Comment