Monday, March 4, 2013

Mauaji siku ya kupiga kura Kenya


Mmoja wa wale waliojeruhiwa
 Taarifa ambazo bado hazijathibitishwa zinasema kuwa watu 10, wakiwemo maafisa wa polisi wawili, wameuawa mjini Mombasa, Pwani ya Kenya. Tukio hilo lilitokea alfajiri, kuamkia leo wakenya wanapopiga kura.
 
Hata hivyo polisi walithibitisha vifo vya maafisa wao wawili vilivyotokea wakati polisi walipowapiga risasi washambulizi waliokuwa wamejihami kwa mapanga. Lilikuwa shambulizi la kulipiza kisasi.
 
Washambulizi hao wanashukiwa kuwa wafuasi wa kundi la Pwani la Mombasa Republican Army (MRC) ambao wamekuwa wakipigania uhuru wa jimbo la Pwani.
 
Mwandishi wa BBC, Karen Allen, anasema polisi waliweza kuthibitisha vifo vya wanne katika eneo la Changamwe, naye Hassan Majid aliona mtu mmoja kauawa eneo la Mishomoroni. Mwtu mwingine Moja ya miili hiyo ilikuwa imekatwakatwa.
 
Zaidi ya watu 1,000 waliuawa miaka mitano iliyopita katika ghasia zilizotokea baada ya uchaguzi wa mwaka 2007.

No comments:

Post a Comment