Katibu Mkuu wa CHADEMA Taifa leo hii anahudhuria Ibada ya Maziko ya Padre Evaristus Mushi aliyeuawa siku ya Jumapili huko Zazinzibar.
Akiongea na Radio Maria kabla ya Misa kuanza Dr. Slaa ameikumbusha Serikali kukumbuka kazi yake Msingi kwa watu wake ambayo ni kulinda Uhai wa Wananchi wake. Akifafanua kauli hiyo amekumbusha matukio kadhaa ya mauaji na mashambulizi yaliyojitokeza hivi karibuni ambayo hadi sasa Serikali haijachukua hatua zozote. amekumbusha matukio ya Padre kunusurika kifo baada ya kupigwa Risasi hapo hapo Zanzibar siku za karibuni, tukio la vurugu za Geita zilizosababisha mauaji ya Mchungaji na Matukio ya Katibu wa Mufti kumwagiwa Tindikali huko Zanzibar.
Pia Slaa ambaye aliwahi kuwa Padre ametoa ufafanuzi wa Kihistoria kuwa Msingi wa Ukristo TAnzania ni Zanzibar kwani Wamisionari wa Kwanza kuingia Afrika Mashariki walianzia Visiwani humo kabla ya kwenda sehemu nyingine, hivyo Kuna ulazima wa kuangalia kwa nini mauaji na Visa vizidi katika kipindi hiki.
Ameikumbusha pia Serikali kufuatilia kiini cha matukio hayo ya mauaji na si kuishia katika kuangalia au kujiuliza juu ya matunda ya mambo ambayo yana msingi wake.
Misa hiyo ya imeongozwa na Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, na kuhudhuriwa pamoja na viongozi Mbalimbali wa kisiasa, serikali na Dini mbalimbali.
No comments:
Post a Comment