NGUVU ZA KIUME, TATIZO LINALOZIDI KUONGEZEKA KILA UCHAO;
- Wahanga ni vijana
- "Misosi ya kijanja", sigara na Ulabu chanzo cha tatizo.
Madaktari wengi wameripoti juu ya kuwepo kwa
ongezeko la wagonjwa wengi wa kiume ambao wamekuwa wakilalamikia juu ya
upungufu wa nguvu za kiume.
Mwaka jana mwishoni gazeti la The Independent llilopo nchini Uingereza liliripoti kuwa hali ya afya ya viungo vya uzazi hususani kwa wanaume ilishuka kwa kiwango kikubwa na hiyo ilitokana na utafiti uliofanywa duniani juu ya ubora wa mbegu za kiume.

Utafiti huo ulionyesha kuwa katika miaka ya 1989
hadi 2005 ulionyesha kuwa kati ya wanaume 26,000 waliofanyiwa uchunguzi
robo tatu yake walionekana kuwa na uwezekano mkubwa wa kushindwa kuzaa.
Mwaka 1989 na 2005, kwa mujibu wa gazeti moja la
Uingereza lilisema kwamba “Wanaume 26,000 wanakabiliwa na tatizo hilo
la upungufu wa mbegu za kiume.’’
Utafiti huo uliendelea kufanyika ili kuhakikisha juu ya uchunguzi uliofanyika miaka 20 iliyopita na matokeo yake yalizidi kuonyesha kuwa nguvu za kiume zimezidi kudhoofika kwa wanaume wengi duniani.
Utafiti huo uliendelea kufanyika ili kuhakikisha juu ya uchunguzi uliofanyika miaka 20 iliyopita na matokeo yake yalizidi kuonyesha kuwa nguvu za kiume zimezidi kudhoofika kwa wanaume wengi duniani.
Miongoni mwa sababu ambazo zimekuwa zikisababisha
nguvu hizo kuporomoka ni pamoja na kuvaaji wa nguo za ndani ambazo
zinabana, pia wataalamu walieleza kuwa ufumbuzi juu ya sababu maalumu
ya nguvu hizo kushuka bado haujapatikana.
Baadhi ya waandishi nchini Kenya hususan katika gazeti la Daily Nation waliamua kufanya utafiti juu ya hilo ili kuweza kufahamu kama tatizo hilo lipo nchini humo.
Baadhi ya waandishi nchini Kenya hususan katika gazeti la Daily Nation waliamua kufanya utafiti juu ya hilo ili kuweza kufahamu kama tatizo hilo lipo nchini humo.
Utafiti huo ulifanywa na daktari mmoja maarufu
katika Hospitali ya Royal Garden nchini humo aliyejulikana kwa jina la
Solomon Wasike ambaye alisema kuwa wiki mbili zilizopita alipata mgonjwa
mwenye tatizo kama hilo.
Aliongeza kuwa mwanamume huyo alikuwa na umri wa
mika 28 alikuwa amefika katika kliniki yake kwa ajili ya kupima juu ya
uwezo wake wa kuzaa.
Hali hiyo ilikuja baada ya kufunga ndoa na mke wake mwaka mmoja uliopita lakini hadi sasa mwanamke huyo alishindwa kupata mimba.
Hali hiyo ilikuja baada ya kufunga ndoa na mke wake mwaka mmoja uliopita lakini hadi sasa mwanamke huyo alishindwa kupata mimba.
Daktari Wasike alisema kuwa baada ya maelezo hayo
aliamua kuchukua mbegu zake mwanaume huyo kwa ajili ya vipimo
aliongeza kuwa majibu yake yalikuwa na utata kwa kuwa yalionyesha kuwa
mtu huyo alikuwa na uwezo mdogo wa kuzalisha mbegu hali ambayo
iliyosababisha mke wake kutopata mimba.
Wasike alisema kuwa hali hiyo imekuwa ikijitokeza
mara kwa mara katika kliniki hiyo kuwa na wagonjwa wengi wa kiume wenye
matatizo katika afya ya uzazi.
“Kinachotusumbua ni kwamba vijana wengi wanaokuja
katika hospitali hii wamekuwa na matatizo sawa katika mbegu za kiume na
jambo hili linazidi kusikitisha kwa kuwa asilimia kubwa ya watu
wanaokuja ni vijana.
Aliongeza kuwa hali hiyo inafanya tuamini kuwa
licha ya wengine kuwa na matatizo hayo tangu kuzaliwa lakini asilimia
kubwa ya vijana wanapatwa na tatizo hilo kwa sababu ya hali ya maisha
wanayopitia pamoja na mazingira wanayoishi.
Hata hivyo takwimu za kitaifa bado hazijafanywa
juu ya tatizo licha ya kuwa kumekuwa na malalamiko mengi ya wanaume
kutoka katika katika hospitali mbalimbali.
Pia kuna takwimu kutoka katika kituo cha afya Nairobi IVF
Centre, ambacho ni mojawapo kati vituo ambavyo uhusika na upimaji wa
mbegu za kiume kwa kiasi kikubwa ambao nao pia waleleza kuwa kiwango
kidogo cha mbegu za kiume ambazo pia huwa ni dhoofu kimezidi kujitokeza
kwa baadhi ya wanaume wengi nchini humo.
Dk Joshua Noreh ambaye alikuwa anahusika na
upimaji pamoja na utoaji wa huduma katika kituo hiko alisema kuwa
wastani wa wanaume ambao wanatembelea katika kituo hiko huwa na umri wa
miaka 35.
Aliongeza kuwa kwa mujibu wa data kutoka katika
kituo chake asilimia 14 ya wanaume ambao mbegu zao zilifanyiwa utafiti
zilionyesha kuwa wamekuwa na tatizo hilo.
Aliongeza kuwa hali hiyo imezidi kwa asilimia tatu.
Aliongeza kuwa hali hiyo imezidi kwa asilimia tatu.
Miaka mitatu iliyopita asilimia 11 ya wanaume
walionekana kuwa na tatizo hiyo hali ambayo imeonyesha kuwa tatizo hilo
limekuwa likikua kila baada ya mwaka mmoja.
Kwa mujibu wa maelezo kutoka Shirika la Chakula
Duniani (WHO) lilieleza kuwa mwanamume mwenye mbegu za kiume ambazo
hazina matatizo anatakiwa awe na mbegu za kiume kuanzia milioni 10 hadi
20 kwa milimita.
Tatizo hilo la kuwa na mbegu za kiume ambazo ni
dhoofu zinazosababisha kutokuwa na uwezo wa kuzaa husababishwa na
kubadilika kwa hali ya maisha pamoja na kubadilika kwa mazingira.
Daktari huyo aliwataka wanaume kuwa makini na maisha ambayo wanaishi kwa kuwa yanaweza kuathiri utendaji kazi wa mbegu hizo.
Daktari huyo aliwataka wanaume kuwa makini na maisha ambayo wanaishi kwa kuwa yanaweza kuathiri utendaji kazi wa mbegu hizo.
Pia aliwataka wanaume kupunguza uvutaji wa sigara
pamoja na unywaji wa pombe kupitiliza, kula vyakula vya kukaanga vyenye
mafuta kwa kuwa vinaongeza kwa kiasi kikubwa tatizo la kushindwa kuzaa.
Utafiti uliofanywa mwaka 1940 ulionyesha kuwa
asilimia 50 ya nguvu za kiume hushuka kutokana na kiwango kikubwa cha
unywaji wa uvutaji wa sigara, pombe pamoja na mabadiliko ya mazingira.
Pia uvutaji wa sigara 20 kwa siku na ulaji wa chipsi, baga, soseji inachangia kwa asilimia 43 kuharibu nguvu za kiume.
Pia uvutaji wa sigara 20 kwa siku na ulaji wa chipsi, baga, soseji inachangia kwa asilimia 43 kuharibu nguvu za kiume.
Dk Wasike alisema kuwa asilimia kubwa ya wanaume
wanaosumbuliwa na tatizo hilo kutokana na hali ya mazingira wanayoishi
ni wale ambao wanafanya kazi shambani kwa kuwa kuna aina ya madawa
ambayo yanapulizia yanaharibu mbegu hizo.
Pia aliongeza kuwa wanaume ambao wanaendesha
vyombo vya moto na kukaa karibu na injini hizo za magari na wale ambao
wanapakata kompyuta katika mapaja kwa muda mrefu wanahatari kubwa ya
kupata tatizo hilo.
Aliwataka wanaume kula mboga za majani kwa wingi
na matunda na kupunguza ulaji mkubwa wa nyama na maziwa kwa kuwa hivyo
pia ulichangia tatizo hilo.
Vilevile aliwataka wanaume kula vyakula vyenye
virutubisho ambavyo vitasaidia katika kujenga mwili ikiwemo na kuvipa
uwezo mbegu hizo.
Wanaume pia walitakiwa kuacha kuoga kwa kutumia maji ya moto kwa kuwa hupunguza uwezo wa kutengeneza nguvu zao.
Kutoka:www.mwananchi.co.tz
Wanaume pia walitakiwa kuacha kuoga kwa kutumia maji ya moto kwa kuwa hupunguza uwezo wa kutengeneza nguvu zao.
Kutoka:www.mwananchi.co.tz
No comments:
Post a Comment