Taarifa zilizopo ni kuwa mtu mmoja anayeitwa Ali Khamis ambaye ni Imamu
wa Msikiti Mkaazi wa Mwakaje amepigwa mapanga na watu wasiojulikana
huko Kidoto Mkoa wa Kaskazini Unguja jana,
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja, Ahmada Khamis
amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo anasema limetokea majira ya
saa 8 mchana huko Kitope wakati Marehemu akiwa shambani kwake,
Kwa mujibu wa taarifa za polisi zinasema Imamu huyo alipigwa mapanga
shingoni kwake na kupoteza damu na kusababisha kifo chake wakati
akikimbizwa hospitali.
Jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.
No comments:
Post a Comment